Ruka hadi maudhui
Soma Qurani Tukufu katika lugha 49 pamoja na tafsiri na usomaji  Anza kusoma →
Islam Word Quran & Seerah
سُورَةُ ٱلْفَاتِحَةِ
Al-Faatiha — The Opening
Sura 1 · aya 7 · Makki
Usomaji wa sura nzima Mishary Rashid Alafasy
0:00 0:00

Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani

1

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

2

ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;

3

ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu;

4

مَٰلِكِ يَوْمِ ٱلدِّينِ

Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo.

5

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.

6

ٱهْدِنَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلْمُسْتَقِيمَ

Tuongoe njia iliyo nyooka,

7

صِرَٰطَ ٱلَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ ٱلْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا ٱلضَّآلِّينَ

Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.